2 Kiongozi ataingia ndani kupitia njia ya ukumbi wa lango,+ naye atasimama kando ya mwimo wa lango. Makuhani watatoa dhabihu yake nzima ya kuteketezwa na dhabihu zake za ushirika, naye atainama chini kwenye kizingiti cha lango na kutoka nje. Lakini lango linapaswa kubaki wazi mpaka jioni.