-
Yeremia 52:24-27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Mkuu wa walinzi alimchukua pia Seraya mkuu wa makuhani,+ Sefania+ kuhani wa pili, na walinzi watatu wa milango.+ 25 Pia alimchukua kutoka jijini ofisa mmoja wa makao ya mfalme aliyekuwa msimamizi wa wanajeshi, watu saba waliopatikana jijini walioshirikiana kwa ukaribu na mfalme, na pia mwandishi wa mkuu wa jeshi, aliyewaandikisha watu jeshini, na wanaume 60 kutoka miongoni mwa watu wa kawaida waliokuwa bado jijini. 26 Nebuzaradani mkuu wa walinzi aliwachukua na kuwapeleka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla. 27 Mfalme wa Babiloni aliwapiga na kuwaangamiza huko Ribla+ katika nchi ya Hamathi. Hivyo watu wa Yuda wakapelekwa uhamishoni kutoka katika nchi yao.+
-