-
Danieli 2:34, 35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
34 Uliendelea kutazama hadi jiwe likakatwa, si kwa mikono, nalo likaipiga sanamu hiyo kwenye nyayo zake za chuma na za udongo wa mfinyanzi na kuzipondaponda.+ 35 Wakati huo kile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha, na ile dhahabu, vyote pamoja, vikapondwapondwa na kuwa kama makapi kutoka kwenye uwanja wa kupuria wakati wa kiangazi, kisha upepo ukavipeperusha mbali hivi kwamba hakuna chembe yoyote ya vitu hivyo ingeweza kupatikana. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa, nalo likaijaza dunia yote.
-