-
Danieli 3:4-6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Mpiga mbiu akatangaza hivi kwa sauti kubwa: “Enyi watu wa makabila, mataifa, na lugha zote, mnaamriwa kwamba, 5 wakati mtakaposikia sauti ya pembe, zumari, zeze, kinubi cha pembe tatu, kinanda, zumari-tete, na ala nyingine zote za muziki, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza amesimamisha. 6 Yeyote ambaye hataanguka chini na kuabudu atatupwa mara moja katika tanuru lenye moto mkali.”+
-