-
Danieli 4:32, 33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
32 nawe unafukuzwa mbali kutoka kati ya wanadamu. Utaishi na wanyama wa mwituni, nawe utapewa majani ule kama ng’ombe dume, na nyakati saba zitapita, mpaka utakapojua kwamba Aliye Juu Zaidi ni Mtawala katika ufalme wa wanadamu na yeye humpa ufalme huo yeyote anayetaka kumpa.’”+
33 Papo hapo, maneno hayo yakatimia kwa Nebukadneza. Akafukuzwa mbali kutoka kati ya wanadamu, akaanza kula majani kama ng’ombe dume, na mwili wake ukalowa kwa umande wa mbinguni, mpaka nywele zake zikawa ndefu kama manyoya ya tai na kucha zake zikawa kama kucha za ndege.+
-