3 alishauriana na wakuu wake na mashujaa wake na kuamua kuziba chemchemi za maji zilizokuwa nje ya jiji,+ nao wakamsaidia. 4 Watu wengi walikusanywa, nao wakaziba chemchemi zote na kijito kilichopita nchini, wakisema: “Kwa nini wafalme wa Ashuru waje na kupata maji mengi?”