-
Yeremia 7:5-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Mkirekebisha kikweli njia zenu na matendo yenu; mkitekeleza haki kikweli kati ya mtu na jirani yake;+ 6 msipowakandamiza wakaaji wageni, mayatima,* na wajane;+ msipomwaga damu isiyo na hatia mahali hapa; na msipoifuata miungu mingine na kujiletea madhara;+ 7 basi nitawaruhusu mwendelee kukaa mahali hapa, katika nchi niliyowapa mababu zenu daima.”’”*
-
-
Yeremia 25:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Walikuwa wakisema, ‘Tafadhali, geukeni kila mmoja wenu kutoka katika njia zenu za uovu na matendo yenu maovu;+ nanyi mtaendelea kukaa kwa muda mrefu katika nchi ambayo Yehova aliwapa ninyi na mababu zenu zamani. 6 Msiifuate miungu mingine na kuiabudu na kuiinamia, na kunikasirisha kwa kazi ya mikono yenu; la sivyo nitawaletea msiba.’
-