Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Luka 12:22-28
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 22 Kisha akawaambia wanafunzi wake: “Ndiyo sababu ninawaambia, acheni kuhangaikia uhai wenu* kuhusu kile mtakachokula au miili yenu kuhusu kile mtakachovaa.+ 23 Kwa maana uhai una* thamani kuliko chakula na mwili kuliko mavazi. 24 Waangalieni kunguru: Hawapandi mbegu wala hawavuni; hawana bohari wala ghala; lakini Mungu huwalisha.+ Je, ninyi si wenye thamani kuliko ndege?+ 25 Ni nani kati yenu ambaye kwa kuhangaika anaweza kurefusha uhai wake kwa mkono* mmoja? 26 Basi, kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini mhangaikie yale mambo mengine?+ 27 Angalieni jinsi mayungiyungi* yanavyokua: Hayafanyi kazi wala hayasokoti; lakini ninawaambia hata Sulemani katika utukufu wake wote hakupambwa kama maua hayo.+ 28 Basi, ikiwa Mungu huivika hivyo mimea ya shambani, ambayo ipo leo na kesho hutupwa ndani ya jiko, je, hatawavika vizuri zaidi ninyi wenye imani ndogo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki