-
Luka 19:20-23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Lakini mwingine akaja, akasema, ‘Bwana, hii hapa mina yako, niliifunga kwa kitambaa nikaificha. 21 Nilikuogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali; wewe huchukua kile ambacho hukuweka akiba, na kuvuna kile ambacho hukupanda.’+ 22 Akamwambia, ‘Ninakuhukumu kwa maneno yako mwenyewe, mtumwa mwovu. Ulijua, sivyo, kwamba mimi ni mtu mkali, ambaye huchukua kile ambacho sikuweka akiba na kuvuna kile ambacho sikupanda?+ 23 Basi kwa nini hukuziweka pesa* zangu benki? Kisha baada ya kurudi, ningezichukua zikiwa na faida.’
-