-
Mathayo 16:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
16 Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu, na ili kumjaribu wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.+ 2 Akawajibu: “Inapofika jioni ninyi husema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri kwa maana anga ni jekundu,’ 3 na asubuhi mnasema: ‘Leo kutakuwa na baridi kali na mvua, kwa maana anga ni jekundu na lina mawingu mazito.’ Mnajua jinsi ya kufafanua hali ya anga, lakini hamwezi kufafanua ishara za nyakati.
-