6 Lakini yeyote anayemkwaza mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungiwe shingoni jiwe la kusagia ambalo huzungushwa na punda, kisha azamishwe baharini.+
17Ndipo akawaambia wanafunzi wake: “Lazima vikwazo vije. Hata hivyo, ole wake mtu atakayevisababisha! 2 Ingekuwa afadhali kwake kama angefungiwa shingoni jiwe la kusagia kisha atupwe baharini kuliko amkwaze mmoja wa hawa wadogo.+