-
Mathayo 12:43-45Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
43 “Roho mwovu anapomtoka mtu, yeye hupitia maeneo yasiyo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati.+ 44 Kisha anasema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu niliyoihama’; naye anapofika, anakuta haijakaliwa lakini imefagiwa ikawa safi na kupambwa. 45 Naye huenda na kuwaleta roho wengine saba walio waovu kuliko yeye, na baada ya kuingia ndani, wao hukaa humo; na hali ya mwisho ya mtu huyo huwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza.+ Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia kwa kizazi hiki kiovu.”
-