-
Luka 11:24-26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 “Roho mwovu anapomtoka mtu, yeye hupitia maeneo yasiyo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini anapokosa yeye husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu niliyoihama.’+ 25 Anapofika hukuta nyumba ikiwa imefagiwa ikawa safi na kupambwa. 26 Kisha huenda na kuwaleta roho wengine saba walio waovu kuliko yeye, na baada ya kuingia ndani, wao hukaa humo. Basi hali ya mwisho ya mtu huyo huwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza.”
-