-
Yohana 2:1-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Basi siku ya tatu kulikuwa na karamu ya ndoa katika Kana ya Galilaya, na mama ya Yesu alikuwa huko. 2 Yesu na wanafunzi wake pia walikuwa wamealikwa kwenye karamu hiyo ya ndoa.
3 Divai ilipopungua mama ya Yesu akamwambia: “Hawana divai.” 4 Lakini Yesu akamjibu: “Mwanamke, jambo hilo linatuhusuje mimi na wewe?* Bado saa yangu haijafika.” 5 Mama yake akawaambia wahudumu: “Fanyeni lolote atakalowaambia.” 6 Kulikuwa na mitungi sita ya maji hapo kulingana na sheria za utakaso za Wayahudi,+ kila mmoja ulikuwa na uwezo wa kuchukua vipimo* viwili au vitatu vya maji. 7 Yesu akawaambia: “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza pomoni. 8 Akawaambia: “Choteni kidogo na kumpelekea msimamizi wa karamu.” Basi wakampelekea. 9 Msimamizi wa karamu alipoonja maji yaliyokuwa yamegeuzwa kuwa divai, bila kujua divai ilitoka wapi (lakini wahudumu waliokuwa wamechota maji hayo walijua), akamwita bwana harusi 10 akamwambia: “Kila mtu hutoa divai nzuri kwanza, kisha hutoa divai hafifu wakati ambapo watu wameingiwa na kileo. Lakini wewe umehifadhi divai nzuri mpaka sasa.” 11 Yesu alifanya muujiza huo wake wa kwanza katika Kana ya Galilaya, kwa hiyo akaonyesha utukufu wake,+ na wanafunzi wake wakamwamini.
-