18 Basi kulipokucha, kukawa na mvurugo miongoni mwa wanajeshi kuhusu kilichompata Petro. 19 Herode akamtafuta kwa bidii, na aliposhindwa kumpata, akawahoji walinzi na kuamuru wapelekwe kuadhibiwa;+ basi akatoka Yudea na kushuka kwenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.