-
Matendo 19:9, 10Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Lakini baadhi yao wakawa wagumu* na wakakataa kuamini, huku wakizungumza vibaya kuhusu Ile Njia+ mbele ya umati. Basi akawaacha+ na kuwatenga wanafunzi kutoka kwao, na kila siku alikuwa akitoa hotuba katika ukumbi wa shule ya Tirano. 10 Aliendelea kufanya hivyo kwa miaka miwili, hivi kwamba wote walioishi katika mkoa wa Asia wakasikia neno la Bwana, Wayahudi na Wagiriki pia.
-