-
Matendo 21:31-33Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 Walipokuwa wakijaribu kumuua, kamanda wa kikosi cha jeshi akapata habari kwamba Yerusalemu yote ilikuwa na vurugu; 32 mara moja akachukua wanajeshi na maofisa wa jeshi wakakimbia kwenda huko. Walipomwona kamanda wa jeshi na wanajeshi, wakaacha kumpiga Paulo.
33 Ndipo yule kamanda wa jeshi akakaribia akamweka chini ya ulinzi na kuamuru afungwe kwa minyororo miwili;+ kisha akauliza huyo ni nani na alikuwa amefanya nini.
-