24 Nenda pamoja na watu hawa ukajitakase kisherehe pamoja nao na kuwagharimia, ili wanyolewe vichwa vyao. Ndipo kila mtu atajua kwamba uvumi walioambiwa kukuhusu si wa kweli, bali unatembea kwa utaratibu, na pia unashika Sheria.+
26 Ndipo Paulo akaenda pamoja na wanaume hao siku iliyofuata, akajitakasa kisherehe pamoja nao,+ naye akaingia hekaluni ili kutoa taarifa kuhusu wakati ambapo siku za kujitakasa zingekwisha na toleo litolewe kwa ajili ya kila mmoja wao.