-
Matendo 25:10-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Lakini Paulo akasema: “Mimi nimesimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, ambapo ninapaswa kuhukumiwa. Sijawakosea Wayahudi, nawe pia umegundua jambo hilo. 11 Ikiwa, kwa kweli mimi ni mkosaji na nimefanya jambo lolote linalostahili kifo,+ niko tayari kufa; lakini kama mashtaka ya watu hawa hayana msingi, hakuna mtu aliye na haki ya kunikabidhi kwao ili tu apate kibali chao. Ninakata rufaa kwa Kaisari!”+ 12 Ndipo Festo, baada ya kuzungumza na baraza la washauri, akajibu: “Umekata rufaa kwa Kaisari; nawe utaenda kwa Kaisari.”
-