Unaweza Kumtumaini Nani?
Kasisi?
Muuza nyama?
Mwanasheria?
Mwanasiasa?
Udanganyifu umepenya kila namna ya maisha. Bila shaka twahitaji sauti tunayoweza kutumaini.
Mnara wa Mlinzi na Amkeni! ndizo sauti hizo. Unaweza kuzitumaini. Kwa sababu gani? Kwa sababu magazeti hayo yamejitoa yazitegemeze kanuni za haki za Biblia. Hayapendezi watangazaji wa kibiashara. Yasome kwa ukawaida.
Tafadhali mnipelekee uandikishaji wa mwaka mzima wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Nimepeleka Kshs. 83/- ili nipokee matoleo 36 ya magazeti hayo (nakala tatu kila mwezi).