Ensaiklopedia Mpya ya Biblia
Wengi wamekuwa wakiandikia kueleza uthamini wao kwa ensaiklopedia mpya ya Biblia ambayo wamepokea. “Lo, jinsi yale mabuku mapya mawili Insight on the Scriptures yalivyo msaada mzuri ajabu wa kufanyia utafiti!” asisimuka mwandikaji mmoja wa kutoka Wisconsin, U.S.A. “Kweli kweli hiyo ni zawadi nzuri ajabu, moja ambayo mimi nitaithamini milele na kujitahidi kuitumia kikamili,” aandika mwanamke mmoja kutoka Jamaica, West Indies.
Mabuku hayo mawili ya Insight on the Scriptures, yana jumla ya kurasa 2,560 katika chapa zenye kuonekana wazi na kusomeka vizuri. Maelfu ya makala zayo yamepangwa kialfabeti na yana maelezo marefu. Yahusu watu, mahali mbalimbali, uhai wa mimea na wanyama, matukio maarufu, semi za kitamathali katika Biblia, na rekodi ya mishughuliko ya Mungu pamoja na aina ya kibinadamu.
Habari 53 zimekuzwa zikiwa sehemu maalumu kwa rangi kamili. Nyingi zazo ni kutia na ramani na foto za mahali pa kijiografia na mionyesho ya majumba ya makumbusho, na pia michoro mingine ya kukusaidia uyaone akilini masimulizi ya Biblia. Mambo mengine madogo-madogo yenye thamani na maelezo zaidi yameandaliwa kuhusiana na maandiko zaidi ya 3,500 ya Biblia. Faharisi za habari, maandiko, na kupata ramani zimehusishwa.
Pokea ensaiklopedia hii ya mabuku mawili yenye thamani kwa kupeleka hati yenye anwani inayoandama hapa pamoja na Kshs. 280/= (Tshs. 1680/=; RWF 1400.
Tafadhali mnipelekee ensaiklopedia ya Biblia yenye mabuku mawili Insight on the Scriptures. Mimi nawapelekea Kshs. 280/= (Tshs. 1680/=; RWF 1400).