Ukurasa wa Pili
Dunia yetu ndiyo makao ya familia nzima ya kibinadamu. Watu wote huishi juu yayo pamoja na kushiriki mahitaji na tamaa zile zile za msingi.
Hata hivyo, upatano wa jamii za watu wa rangi mbalimbali umekuwa si kawaida juu ya tufe hili. Bali, mara nyingi mno tofauti zilizo miongoni mwa watu ndizo huongoza mahusiano ya kibinadamu. Kwa karne kadhaa ubishi umewaka juu ya mambo ya jamii za rangi mbalimbali. Katika toleo hili la Amkeni!, sisi twakaza fikira juu ya yale ambayo sasa yajulikana juu ya jamii za rangi mbalimbali na kwa nini twaweza kutarajia mwisho wa ugomvi wote kati ya watu wa jamii za rangi mbalimbali.