Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/8 uku. 32
  • “Kwelikweli Nyinyi Mwawajali Wanadamu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kwelikweli Nyinyi Mwawajali Wanadamu”
  • Amkeni!—1993
Amkeni!—1993
g93 2/8 uku. 32

“Kwelikweli Nyinyi Mwawajali Wanadamu”

Huo ndio mkataa aliofikia mwanamume mmoja katika Kalifornia, U.S.A., ambaye hufurahia kusoma vichapo vya Watch Tower Society. Kuhusu kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi aliandika hivi:

“Sasa mimi ninakisoma chote mara ya pili, na sikuzote kinakuwa usomaji wenye kupendeza. Si kwamba tu kitabu hicho ni chenye kufundisha bali pia vielezi vyenye rangi vyaonekana sana kuwa na uhai. Kila picha hunifanya nihisi kana kwamba ninaishi huko nyuma katika wakati wa Yesu.

“Mathalani, yule mwanamume aliyepagawa na roho waovu katika sura ya 45 huonekana akiwa mkali na hatari. Hata hivyo, Yesu aoyeshwa akija ufukoni bila woga na kufukuza roho hao mashetani . . .

“Michoro yote ya viongozi wa Kiyahudi wenye chuki ni sanaa kwelikweli. Zaonyesha jinsi mtu awezavyo kuonekana kuwa na hasira alazimikapo kushughulika na Yesu na bado hataki kuacha njia zake zenye dhambi. Ningeweza kuendelea kutaja mengi. . . . Kwelikweli nyinyi mwawajali wanadamu . . .

“Mimi si mmoja wa Mashahidi wa Yehova lakini hupenda kupokea Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi hungojea kwa hamu kila toleo, na liwasilipo, ndiyo sehemu bora zaidi ya barua zangu. Amkeni! la Juni 22 (Kiingereza) ni mshindi wa zawadi! ‘Kulea Watoto Katika Ulimwengu Usio na Adili’ ilikuwa habari yenye kuufaa sana wakati huu . . .

“Nina miaka 35 nami nimekuja kung’amua kwamba ulimwengu huu wa kale unakabili matatizo makubwa. Nina furaha kwamba mko huko nje mkisema kweli juu ya ulimwengu wa kale na jinsi Mungu ahisivyo juu yao.”

Mashahidi wa Yehova ni tengenezo la kimataifa la Wanafunzi wa Biblia zaidi ya milioni nne ambao wamejitoa kusaidia watu wajifunze zaidi juu ya makusudi ya Mungu. Ikiwa ungependa habari zaidi kuhusu Mashahidi wa Yehova na imani zao, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

[Picha katika ukurasa wa 32]

THE GREATEST MAN WHO EVER LIVED

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki