Walitaka Nakala Zao Binafsi
MMOJA wa Mashahidi wa Yehova anayefanya kazi katika Kiwanja-Ndege cha Milan Linate nchini Italia alienda kazini na kile kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Wafanyakazi wenzake kadhaa wakasema wangependa kupata nakala zao binafsi za kichapo hiki kinachozungumzia maisha ya Yesu Kristo. Siku kadhaa baadaye, Shahidi huyo alipopeleka vitabu hivyo vilivyoagizwa, mmoja wa wafanyakazi wenzake akamwambia kwamba wafanyakazi wa mashirika kadhaa ya ndege walisema kwamba wao pia wangependa kupata kitabu hicho. Kwa hiyo yule Shahidi akamwomba atayarishe orodha ya wale wote waliotaka vitabu. Siku kadhaa baadaye alipewa orodha hiyo.
Vitabu vyote vilivyoagizwa havikupatikana mara hiyo, lakini majuma mawili baadaye yule Shahidi alikuwa amevipata. Yeye na Shahidi mwingine wakamtembelea kila mtu aliyekuwa kwenye orodha hiyo, na jumla ya vitabu 461 viliangushwa! Vitabu hivyo vilipokuwa vikiangushwa, mipango ilifanywa kwa watu 13 watembelewe na Mashahidi wanaoishi karibu ili kuanzisha mafunzo ya Biblia nyumbani pamoja nao.
Kama ungependa kupokea nakala ya kitabu hiki chenye jalada gumu na kilicho na kurasa 448 au kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani yoyote ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.