Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 9/22 uku. 32
  • Mahali Wageni Huonyeshwa Ukaribishaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahali Wageni Huonyeshwa Ukaribishaji
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 9/22 uku. 32

Mahali Wageni Huonyeshwa Ukaribishaji

Katika Septemba 1994, mwanamume mmoja kutoka Michigan, Marekani, aliandikia kutaniko la Mashahidi wa Yehova katika Lebanon, Tennessee. Yeye alieleza hivi:

“Huko nyuma Jumapili, Juni 6, 1993, nilihudhuria hotuba yenu ya watu wote na Funzo la Mnara wa Mlinzi. Ilikuwa mara ya kwanza niliyopata kuingia Jumba la Ufalme, na nilipendezwa sana na hizo nyuso zote zenye kutabasamu na upendo wa moyo mweupe nilioonyeshwa. Nilifika nikiwa nimechelewa dakika chache na nilipokaribishwa, niliketi peke yangu. Mume na mke wachanga katika safu iyo hiyo waliniazima Biblia na hatimaye nakala ya gazeti la Mnara wa Mlinzi kwa ajili ya funzo.

“Baada ya mikutano wengi wenu walizungumza nami, tukasalimiana, na kufanya nifurahie kukaa kwangu. Nilipoondoka mwishowe katika Jumba la Ufalme lenu, nilichukua vitabu vitatu—Biblia, Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi, na Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Usiku huo nilisoma sehemu kubwa ya kitabu Kuishi Milele, na nikajifunza jina jipya la Mungu wangu, Yehova. . . .

“Nataka nyote mjue jinsi nilivyothamini ukaribishaji wenu wa ajabu kwa mtu aliye mgeni kabisa na hasa nataka mjue kwamba . . . nilibatizwa Julai 9, 1994, katika umri mchanga wa miaka 70.”

Ikiwa ungependa kupokea ukarimu mchangamfu kutoka wale wanaofurahia kumtumikia Mungu, tafadhali andikia I. B. S. A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani yoyote ifaayo iliyoodhoreshwa kwenye ukurasa 5. Watakujulisha Jumba la Ufalme lililo karibu na kwako.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki