Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 7/22 uku. 32
  • Alichotafuta Ni Ufuatiaji wa Haki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Alichotafuta Ni Ufuatiaji wa Haki
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 7/22 uku. 32

Alichotafuta Ni Ufuatiaji wa Haki

Mwanamke mmoja kijana katika Ekuado alienda kuhojiwa kwa ajili ya kazi. Baada ya kuzungumza na wataka-kazi wengine—wote walikuwa 36—alitambua kwamba ilikuwa vigumu kwake kupata kazi. Wao walikuwa na uzoefu wa kazi na elimu ya chuo kikuu, ilhali yeye hakuwa na yoyote kati ya hizo. Na kati ya maswali sita yaliyoulizwa, alikosa kujibu mawili kwa usahihi. Hata hivyo, swali moja lilikuwa la kibinafsi: “Kweli yamaanisha nini kwako?”

Mwanamke huyo alijibu hivi: “Kweli si dhana tu bali ni kitu ambacho twapaswa kuzoea. Twapaswa kusema kweli na kutodanganya, kwa kuwa tukidanganya, twamfuata Shetani Ibilisi. Tukisema kweli, twampendeza Mungu na kupata manufaa nyingi za kibinafsi.”

Meneja alipouliza juu ya dini ya mwanamke huyo, yeye alijibu kwamba alikuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Siku iliyofuata alijulishwa kwamba alikuwa amechaguliwa kwa kazi hiyo. Mwezi mmoja baadaye mwanamke huyo alimwuliza meneja kwa nini alimteua, naye akasema kwamba ilikuwa kwa sababu ya ufuatiaji wake wa haki.

Je, si kweli kwamba watu wengi leo hawafuatii haki? Kwa upande ule mwingine, watu wanaoistahi Biblia wanatambuliwa kwa ufuatiaji wao wa haki. Mnara wa Mlinzi la Julai 1, 1995, lilisema hivi: “Katika Biblia, kamwe “kweli” si jambo la kuwaziwa tu, lisiloonekana ambalo wanafalsafa hujadili.”

Utanufaika kutokana na usomaji wa kawaida wa Mnara wa Mlinzi, ambalo hutambuliwa ulimwenguni pote kuwa mtetezi wa kweli ya Biblia. Ikiwa ungependa kupata nakala au kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo katika ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki