Je, Wajua?
(Majibu kwa maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 25. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni nini kilichomzuia Yesu kufanya kazi zenye nguvu miongoni mwa watu katika eneo la nyumbani kwao? (Marko 6:5, 6)
2. Ni mimea gani miwili ambayo ilitajwa na Yesu akirejezea utoaji wa sehemu ya kumi wenye kulemea wa Mafarisayo? (Luka 11:42)
3. Ni mnyama gani aliyetumika kiunabii kuonyesha jinsi Yesu angesimama ‘bila kufunua kinywa chake’ alipokuwa akiteswa? (Isaya 53:7, NW)
4. Ni nani aliyekuwa kuhani mkuu ambaye alipokea hukumu kali kwa sababu aliheshimu wana wake zaidi ya Yehova? (1 Samweli 2:27-29)
5. Ni nini ambacho Yesu ‘alikikemea,’ kikamtoka mama-mkwe wa Simoni hivi kwamba akapata nafuu? (Luka 4:38, 39)
6. Sehemu ya kwanza ya mwandamano huitwaje? (Kutoka 14:19)
7. Asili ya uhai wa mwanadamu wa muda tu hufananishwa na nini, kinyume na udumifu wa “usemi wa Yehova”? (1 Petro 1:24, 25)
8. Ni katika eneo gani la jangwa ambapo Waisraeli walikula mana kwa mara ya kwanza na sheria ya Sabato kuanza kutekelezwa? (Kutoka 16:1, 13-31)
9. Ni baadhi ya mambo gani ambayo sanamu haziwezi kufanya? (Zaburi 115:5-7)
10. Kwa sababu walikosa kumtukuza na kumheshimu Mungu kwenye maji ya Meriba, ni nani ambao hawakuruhusiwa kuingia katika Bara Lililoahidiwa? (Hesabu 20:12)
11. Ni sehemu gani ya mwili ambayo hutumika kwa njia ya mfano kuwakilisha uwezo wa kutumia nguvu? (Isaya 51:9)
12. Akionyesha ukuu wa ukuhani wa Kristo, Paulo alisema Lawi alilipa nini alipokuwa angali katika viuno vya Abrahamu? (Waebrania 7:9, 10)
13. Ni usemi gani utumiwao katika Biblia kuonyesha kwamba mfalme wa Israeli aliwakilisha utawala wa Yehova wa kitheokrasi? (1 Mambo ya Nyakati 29:23)
14. Kila mmoja wa wale viumbe hai wanne katika ono la Yohana aliwakilisha nini? (Ufunuo 4:7)
15. Ni nini kilipaswa kupata dunia baada ya Ibilisi kutupwa kutoka mbinguni? (Ufunuo 12:12)
16. Ni nini kilichotumiwa kugawanya Bara Lililoahidiwa miongoni mwa makabila 12? (Hesabu 26:55, 56)
17. Ni ndege yupi aliye na macho yote mawili yakitazama mbele, yakimwezesha kuona kitu kwa macho yote mawili kwa wakati uleule? (Zaburi 102:6)
18. Ni nini ambacho Timotheo angedhihirisha kwa wengine kwa kuendelea kujivama katika mambo ya kiroho? (1 Timotheo 4:15)
19. Danieli alikuwa na wadhifa gani katika serikali ya Babiloni? (Danieli 2:48)
20. Adamu na Hawa walishona nini ili kutengeneza mavazi? (Mwanzo 3:7)
21. Katika kukazia hoja yake ya kutotumia ulimi vibaya, ni nini ambacho Yakobo alisema mtini haungeweza kutokeza? (Yakobo 3:12)
22. Wagonjwa walihitaji kugusa tu sehemu gani ya vazi la Yesu ili wapone kabisa? (Mathayo 14:36)
23. Magimba ya kimbingu yangetumika yakiwa ishara za nini? (Mwanzo 1:14)
24. Ni nani hasa waliokuwa na sifa ya kuwa wenye kiasi, wenye maisha yenye kustahiwa na kazi njema? (Tito 2:2, 3)
25. Isaya alisema kwamba watu watasamehewa nini, ili kwamba “hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa”? (Isaya 33:24)
26. Ingawa andiko alilolinukuu, Zaburi 140:3 (NW), lilimwita “vipiri mwenye pembe” ni jina gani la kawaida kwa nyoka huyo mwenye sumu alilotumia Paulo? (Waroma 3:13)
27. Ni ipi herufi ya sita ya alfabeti ya Kiebrania?
28. Ni usemi gani utumiwao kutofautisha mtu asiye Myahudi? (Waroma 2:9, 10; ona King James Version.)
29. Ni lipi lililokuwa jina la bandari ya Italia ambapo Paulo alitumia juma moja pamoja na Wakristo wenzake alipokuwa njiani kuelekea kusimama mbele ya Kaisari? (Matendo 28:13, 14)
30. Paulo hutushauri kuweka macho yetu kwa mambo gani yadumuyo milele? (2 Wakorintho 4:18)
31. Wakristo hawapaswi kujifanyia nini, kwa kuwa kitashughulikiwa na Yehova? (Waroma 12:19)
32. Katika kukazia hali ya kuharibu ya Gehena, Yesu alisema ni nini ambacho hakifi huko? (Marko 9:48)
Majibu ya Maswali
1. Ukosefu wao wa imani
2. Mnanaa, mchicha
3. Kondoo-jike
4. Eli
5. Homa yake
6. Mbele
7. Nyasi inyaukayo
8. Bara la Sini
9. Kusema, kuona, kusikia, kusikia harufu, kushika, kutembea
10. Musa na Haruni
11. Mkono
12. Sehemu za kumi
13. ‘Kuketi katika kiti cha enzi cha BWANA’
14. Simba, fahali, mwanadamu, tai
15. Ole
16. Kwa kura
17. Bundi
18. Kusonga mbele kwake
19. Liwali mkuu
20. Majani ya mtini
21. Zeituni
22. Upinde wenye matamvua
23. Majira, siku, miaka
24. Wanaume na wanawake wenye umri mkubwa
25. Uovu wao
26. Swila mdogo
27. Waw
28. Mtu wa mataifa
29. Puteoli
30. “Vitu visivyoonekana”
31. Kutafuta kisasi
32. “Funza wao”