Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 3/22 uku. 32
  • Gazeti Lenye Thamani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gazeti Lenye Thamani
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 3/22 uku. 32

Gazeti Lenye Thamani

MUUGUZI mmoja wa London aliandika maneno yafuatayo kwa wachapishaji wa Amkeni!:

“Siku moja nilikuwa nikizungumza na jirani yangu mgeni, Jackie, kuhusu kazi yangu na watu walio wazee-wazee. ‘Nina magazeti ambayo wanaweza kupenda kusoma,’ Jackie akaniambia. Nilipeleka magazeti yake kazini na kuyaacha kwenye meza. Katika ziara za baadaye nilipata kwamba yalikuwa yameshikwa-shikwa sana, kumbe watu wamekuwa wakiyasoma.

“Baadaye nilibadili kazi yangu na kuanza kufanya kazi katika hospitali moja. Nikaweka baadhi ya magazeti ya jirani yangu katika chumba cha kungoja. Tena niliona yalikuwa yakisomwa. Asubuhi moja nilipokuwa nikishughulikia mkono wa bibi mmoja mzee-mzee, mume wake alisema: ‘Natumaini inaruhusiwa, nilichukua gazeti hili katika chumba cha kungoja. Lina makala nzuri sana ambayo nataka kumwonyesha mwana wangu.’

“Magazeti hayo yamekuwa baraka kwangu pia. Kwa kuwa bado nazoezwa uuguzi, nimetumia habari zilizo katika makala hizo katika maandishi yangu ya utafiti, nikipata itikio zuri la walimu wangu.

“Jirani yangu Jackie ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, na gazeti ambalo nimekuwa nikirejezea ni Amkeni! Yale ambayo nimesoma katika gazeti hili yamenisaidia kuelewa mengi kujihusu na kuhusu wakati ujao wa wanadamu.”

Kama ungependa kupokea matoleo ya wakati ujao ya Amkeni!, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova wa kwenu au andika kwa kutumia anwani iliyo karibu zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki