Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 11/22 uku. 32
  • Je, Dini Zote Huelekeza kwa Mungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Dini Zote Huelekeza kwa Mungu?
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 11/22 uku. 32

Je, Dini Zote Huelekeza kwa Mungu?

Mamilioni ya watu huamini kwamba dini zote ni barabara mbalimbali zinazoelekeza mahali pamoja. Ukweli ni kwamba, yale mafundisho, desturi, na miungu ya dini nyingi hufanana. Mathalani, tazama sanamu hii ya kihekaya ya karne ya nane W.K. ya Wahindu, kutoka Kerala, India.

Jambo la ajabu ni kuwa fahali waliabudiwa katika dini nyingi za kale. Kwa mfano, kulingana na Diodorus Siculus aliyekuwa mwanahistoria Mgiriki wa karne ya kwanza K.W.K., mungu wa Waamoni Moleki alikuwa pia na umbo la binadamu lakini kichwa cha fahali.

Kwa nini kumekuwa na mifanano sana katika dini mbalimbali ulimwenguni pote? Je, dini hizi zina asili moja? Je, ni barabara mbalimbali zinazoelekea mahali pamoja? Je, Mungu anazikubali zote?

Simulizi lenye kuvutia sana juu ya asili na ukuzi wa zile dini kubwakubwa duniani lililo katika kitabu Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu lajibu maswali kama hayo. Ikiwa ungependa kupokea kitabu hiki au mtu fulani akutembelee nyumbani mwako ili kuzungumzia yale ambayo Biblia yasema kuhusu suala hili, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki