Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 7/22 uku. 32
  • ‘Zinapanua Maarifa Yetu’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Zinapanua Maarifa Yetu’
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 7/22 uku. 32

‘Zinapanua Maarifa Yetu’

Mkuu wa idara ya lugha za kigeni kwenye Taasisi ya Usimamizi ya Karakol katika Kyrgyzstan, ambayo zamani ilikuwa mojawapo jamhuri za Muungano wa Sovieti, alisifu vichapo vya Mashahidi wa Yehova. Aliandika yafuatayo kwa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi:

“Vitabu vyenu na broshua zenu hutusaidia sana kufundisha Kiingereza, Kijerumani, Kirusi, Kikyrgyz na Kituruki chini ya hali za leo zenye mvurugo wa kijamii na kiuchumi. . . . Broshua zenu zinapendwa sana na wale wanaojifunza kazi ya utafsiri . . . Asanteni kwa vitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?, Siri ya Kupata Furaha ya Familia, na Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi.

“Tuna Mashahidi wa Yehova wengi miongoni mwa wanafunzi. Wao hupendezwa sana kusoma makala za Amkeni! na kuzitumia kufanya masomo ya nyumbani.”

Mwandikaji huyo hasa alisifu Amkeni! akisema: “Asanteni kwa makala zenye kupendeza na zenye kuarifu. . . . Zinatupa tumaini na kupanua maarifa yetu ya kawaida. . . . Sisi sote husoma kwa furaha sehemu ya Amkeni! ya ‘Kuutazama Ulimwengu.’”

Kama ungependa kupokea nakala ya Amkeni! au ungependa mmoja wa Mashahidi wa Yehova akutembelee ili kuzungumzia Biblia pamoja nawe, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ihusuyo kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki