Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 2/8 uku. 32
  • Uamuzi Ambao Hutajutia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uamuzi Ambao Hutajutia
  • Amkeni!—1999
Amkeni!—1999
g99 2/8 uku. 32

Uamuzi Ambao Hutajutia

MAMIA ya mamilioni ya wanaume na wanawake waliozaliwa baada ya Vita ya Ulimwengu ya Pili sasa wamefikia umri wa makamo. Ingawa wengi wanaona kuwa wameridhika na yale ambayo wametimiza, baadhi yao wametamaushwa. Wameoa, wamefanya kazi, wamezaa watoto, na kutunza familia, na baadhi yao wamewaona wazazi wao wakifa. Leo, nywele zao zigeukapo kuwa mvi, wanaponenepa, na magoti yao yaanzapo kutoa sauti ya kukwaruzana, wengine huona kwamba wameshindwa kufikia miradi yao maishani. Wakiwa katika hali ya kuvunjika moyo, huenda wakauliza, ‘Ni nini kusudi la uhai?’ Labda hata wewe umeuliza swali hilo.

Kwa hakika ni jambo lenye thamani kubwa kutafakari juu ya maisha yako mara kwa mara. Kwa upande mwingine, kuzingatia maamuzi ambayo unayajutia huenda kukakutia katika hali ya kuvunjika moyo. Badala ya kujiambia, ‘Laiti ninge . . . ,’ ingekuwa vizuri zaidi kukaza fikira kwa maamuzi yafaayo ambayo bado unaweza kuyafanya wakati ujao. Uamuzi kama huo ungekuwa kuchunguza habari inayojibu maswali kuhusu kusudi la uhai. Hivyo, tunakualika usome kichapo Je! Kweli Mungu Anatujali? Kamwe hutajuta ukikubali mwaliko wetu.

Unaweza kupokea broshua hiyo yenye kurasa 32 kwa kujaza kuponi iliyopo hapa na kuipeleka ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani inayohusu iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nipelekeeni nakala ya broshua Je! Kweli Mungu Anatujali?

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki