Iliokoa Fedha za Mtu Huyu
Mwanamume mmoja alipokuwa akisafiri kwa basi kati ya majiji katika Nigeria, Afrika Magharibi, alizungumza na msafiri mwenzake juu ya somo “Mazoea Ambayo Mungu Huchukia,” katika broshua Mungu Anataka Tufanye Nini? Basi liliposimama kwenye hoteli moja, yule mtu aliyependezwa na ile broshua alionyesha furushi alilokuwa amebeba na kueleza: “Hizi ni fedha. . . . Nilizichukua kutoka kwa mojawapo ya mizigo ya safari iliyoko nyuma ya basi.”
Hata hivyo, yule mtu aliyezichukua fedha hizo sasa alisikitikia tendo lake naye alitaka kumrudishia mwenyewe fedha hizo. Furushi hilo lilikuwa la mfanya-biashara mmoja kijana aliyekuwa akisafiri kwa basi hilo. Lilikuwa na kiasi cha naira 150,000 (karibu dola 1,700). Huyo mwizi aliyekuwa akimfuata huyo mfanya-biashara kwa kilometa zipatazo 500, alimwambia huyo mfanya-biashara kijana kwamba anapaswa kumshukuru yule aliyezungumza naye habari iliyo katika broshua. Ni habari hiyo, iliyomfanya arudishe fedha hizo, yeye akaeleza.
Wakati dereva na wasafiri wengine walipojua kilichokuwa kimetendeka, walishangaa, nao wote wakaomba nakala za broshua hiyo. Hapo awali mfanya-biashara huyo hakukubali kamwe kuzungumza na Mashahidi, lakini sasa alitaka funzo la Biblia.
Unaweza kupokea broshua hii yenye faida iliyo na kurasa 32 kwa kujaza na kupeleka kuponi iliyopo hapa ukitumia anwani iliyoonyeshwa, au anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.
□ Nipelekeeni broshua Mungu Anataka Tufanye Nini?
□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.