Ufahamu Wenye Kina Juu ya Ulimwengu Wetu
UFAHAMU huo hupatikana katika kile kitabu kipya Je, Kuna Muumba Anayekujali? katika sura yake yenye kichwa “Ulimwengu Wetu Ulitokeaje?—Ubishi Uliopo.” Lakini kina mengi zaidi. Kitabu hicho huchunguza uhai ulivyoanza—iwe ni kwa nasibu au uliumbwa.
Profesa mmoja wa fizikia huko Marekani alisema hivi: “Kitabu hicho huzungumzia baadhi ya mafumbo yenye kutokeza zaidi katika astrofizikia, biolojia ya molekuli, na mwili wa binadamu, mambo ambayo ni vigumu kuyaeleza kwa kutumia nasibu. Huonyesha waziwazi masuala yanayohusika bila kutatanishwa na mambo magumu ya kiufundi. Kitabu hiki husababu na msomaji na hunukuu wanasayansi mashuhuri katika nyanja mbalimbali. Hiki ni kitabu ambacho mtu anayependezwa kujua mwanzo wa ulimwengu na uhai ni ‘lazima asome,’ awe mwanasayansi au mtu wa kawaida.”
Unaweza kupokea nakala ya kitabu hiki chenye jalada nyepesi cha kurasa 192 kwa kujaza na kupeleka kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ihusuyo iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.
□ Nipelekeeni kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali?
□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.
[Picha katika ukurasa wa 32 zimeandaliwa na 32]
J. Hester and P. Scowen (AZ State Univ.), NASA