Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 2/22 uku. 32
  • Kuwasaidia Watu Kushinda Magumu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuwasaidia Watu Kushinda Magumu
  • Amkeni!—2001
Amkeni!—2001
g01 2/22 uku. 32

Kuwasaidia Watu Kushinda Magumu

OFISI ya tawi ya Mashahidi wa Yehova huko Sri Lanka ilipokea barua kutoka kwa mwandishi wa Sosaiti ya Usitawi wa Wafanyakazi na Vijana, Mkoa wa Mashariki. Mwandishi huyo aliomba matoleo fulani ya awali ya Amkeni! na kusema hivi:

“Mimi na wafanyakazi wenzangu tumeona kwamba magazeti mliyonitumia yanaelimisha, yanaarifu, pia yanachochea na vilevile yanapatana na akili na yanasadikisha. Magazeti hayo hayatangazi fundisho la Kikristo yakiwa na nia yoyote mbaya, kama watu fulani wanavyoweza kudai kimakosa. Nayaona kuwa vichapo bora sana.

“Kuna uhitaji mkubwa sana wa nakala za Amkeni! (mpya na za zamani) na kuna dalili za wazi kwamba uhitaji huo utazidi kuongezeka katika miezi ya usoni. Makala zilizo kwenye magazeti yenu huelimisha wazee, vijana, na watoto. Huwasaidia wote kushinda magumu ya wakati huu na ya wakati ujao yanayotokana na hali za kilimwengu.”

Hakuna pindi nyingine katika historia ambapo watu wa umri wote wamekabili magumu kama leo. Wengi hasa wanataka kujua hali yao ya wakati ujao itakuwaje na kama kuna Mungu anayewajali. Majibu yanayoridhisha ya maswali hayo yanapatikana katika broshua Je! Kweli Mungu Anatujali? Waweza kupokea nakala ya broshua hii kwa kujaza na kutuma kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni nakala ya broshua Je! Kweli Mungu Anatujali?

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki