Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 10/8 uku. 32
  • Jinsi Amkeni! Lilivyookoa Uhai Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jinsi Amkeni! Lilivyookoa Uhai Wake
  • Amkeni!—2001
Amkeni!—2001
g01 10/8 uku. 32

Jinsi Amkeni! Lilivyookoa Uhai Wake

“SIKUTAKA kuendelea kuwa mzigo kwa familia yangu, basi nikaamua kujiua.” Ndivyo alivyoandika mwanamume mmoja kutoka Nepal. Yeye aliendelea hivi: “Nilitayarisha kamba kisha nikachagua mahala na tarehe ya kujiua. Lakini juma moja tu kabla ya siku hiyo, nilipokea toleo la Amkeni! la Februari 22, 2000.”

Toleo hilo lilikuwa na mfululizo wa makala wenye kichwa “Kujiua—Ni Nani Walio Hatarini Zaidi?” Mwanamume huyo aliandika hivi: “Nilijikakamua sana kuchukua gazeti hilo na kulisoma. Maelezo kuhusu mambo kumi yanayochangia kujiua yalinigusa sana na kunifanya nibadili nia yangu.” Yeye alimalizia hivi: “Ni lazima niseme jinsi ninavyothamini yale mliyonifanyia. Jitihada zenu za kuandika makala hiyo ziliokoa uhai wangu!”

Mambo mengi huchangia visa vya kujiua vinavyoongezeka siku hizi. Jambo moja ni kwamba watu wengi sana wamekosa kusudi maishani. Broshua Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje? imewasaidia wengi kujua kwamba kweli kuna tumaini la kupata maisha bora. Waweza kuomba nakala kwa kujaza na kutuma kuponi iliyo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni nakala ya broshua Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje? Onyesha lugha unayotaka.

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki