Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 4/8 uku. 32
  • Walikuwa Wakitazamwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Walikuwa Wakitazamwa
  • Amkeni!—2002
Amkeni!—2002
g02 4/8 uku. 32

Walikuwa Wakitazamwa

WAVULANA wawili waliingia kwenye mkahawa katika mji mdogo huko Ohio, Marekani, ili wapate kiamsha-kinywa. Kama ilivyokuwa desturi yao, kabla ya kula waliinamisha vichwa vyao na kutoa sala kimoyomoyo.

Baadaye, mwanamke mmoja aliyekuwa akiwaona akaja kwenye meza yao na kuchukua karatasi yao ya kudai malipo. Yeye aliwaambia hivi: “Katika ulimwengu ambamo sisi husikia mambo mengi mabaya kuhusu vijana wetu, kuona vijana wawili walio na wakati wa kumshukuru Mungu kwa ajili ya chakula ni jambo lenye kupendeza. Nitalipia kiamsha-kinywa chenu.”

Wavulana hao walishangaa sana, hata hivyo walimshukuru mwanamke huyo. Baadaye walionelea kuwa wasingemwacha afikiri kwamba walikuwa wanasali kwa Mungu yeyote tu. Kwa hiyo mmoja wao akamwendea na, baada ya kumshukuru tena, akamweleza kwamba walikuwa Mashahidi wa Yehova.

Ni desturi ya Mashahidi wa Yehova kujifunza Biblia pamoja na familia zao. Wazazi wa wavulana hao walikuwa wamefanya hivyo. Kitabu kimojawapo ambacho walijifunza kilikuwa Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Kati ya zile sura 19 zilizopo katika kitabu hicho, kuna sura moja inayohusu sala, nayo ina kichwa hiki “Jinsi Unavyoweza Kumkaribia Mungu.”

Unaweza kuomba nakala ya kichapo hicho cha kujifunza Biblia chenye kurasa 192 kwa kujaza kuponi iliyo hapa chini na kuituma kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni nakala ya kitabu Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele.

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki