Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 10/8 uku. 32
  • Mwalimu wa Mambo ya Angani Alivutiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwalimu wa Mambo ya Angani Alivutiwa
  • Amkeni!—2002
Amkeni!—2002
g02 10/8 uku. 32

Mwalimu wa Mambo ya Angani Alivutiwa

Alivutiwa na nini? Na kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali? Mwalimu mmoja kutoka Novo-Sakmarsk, Urusi, aliandikia ofisi ya tawi nchini humo. Aliomba habari zaidi, na kusema:

“Siku chache zilizopita nilikutana na rafiki yangu wa muda mrefu, kisha nikamtembelea. Kitabu kimoja kilichokuwa katika rafu yake ya vitabu kilinivutia sana. Nilipendezwa na kichwa cha kitabu hicho Je, Kuna Muumba Anayekujali?—lakini nilivutiwa hasa na picha iliyo kwenye jalada. Mimi ni mwalimu wa fizikia na mambo ya angani. Nilipokiangalia kitabu hicho, nilipendezwa na habari chungu nzima zilizomo. Kwa vizazi vitatu familia yetu haijazungumza kuhusu dini hata kidogo. Nyanya ya mama yangu alikuwa mtu wa kidini, lakini nyanya yangu alikuwa Mkomunisti, nao (Wakomunisti) hawakuamini Muumba.

“Nikiwa mwalimu wa mambo ya angani, ninawajibika kuwaeleza watoto maoni mbalimbali kuhusu chanzo cha ulimwengu. Nilikisoma kitabu chote, kisha nikaamua kuwatumia barua hii yenye anwani yangu. . . . Pia, niliazima Biblia ili nichunguze maandiko yaliyomo.

“Asanteni sana kwa kitabu hicho! Huenda nimechelewa kutuma barua hii, kwani kitabu hicho kilitolewa katika mwaka wa 1998, hata hivyo natumaini bado ninaweza kupokea habari zaidi kutoka kwenu.”

Wewe pia unaweza kuomba kitabu hicho chenye kurasa 192 kwa kujaza kuponi iliyo hapa na kuituma kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni kitabu Je, Kuna Muumba Anayekujali?

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

J. Hester and P. Scowen (AZ State Univ.), NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki