Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 10/22 uku. 32
  • ‘Yaelekea Liliokoa Uhai Wangu!’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Yaelekea Liliokoa Uhai Wangu!’
  • Amkeni!—2002
Amkeni!—2002
g02 10/22 uku. 32

‘Yaelekea Liliokoa Uhai Wangu!’

“NILIPUUZA dalili nilizokuwa nazo,” asema Claus, ambaye alikuwa akipumua kwa shida sana kwa majuma kadhaa. Lakini jambo fulani lilitukia ambalo lilibadili maoni yake.

“Mimi huweka matoleo ya zamani ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwenye meza iliyo karibu na kitanda changu,” asema Claus. “Jioni moja nilichukua Amkeni! la Machi 22, 2001, na bila kukusudia nikafungua makala yenye kichwa ‘Maajabu ya Mfumo wa Mzunguko wa Damu.’ Niliposoma makala hiyo, nilitambua mara moja kwamba nilikuwa na dalili za ugonjwa wa angina.”

Bila kukawia, Claus alienda hospitali ya karibu ili kupimwa, na ikagunduliwa kwamba mishipa yake ya moyo ilikuwa na tatizo. Alianza kutibiwa mara moja. Daktari alimwambia Claus kwamba anapaswa kushukuru kwa sababu iwapo hangetibiwa, ugonjwa wake ungesababisha mshtuko wa moyo na labda angekufa. Claus aliwaandikia hivi waandishi wa gazeti hili: “Yaelekea Amkeni! liliokoa uhai wangu!”

Gazeti Amkeni! huzungumzia mengi mbali na maajabu ya uumbaji kama vile utendaji wa mwili wa mwanadamu. Kusudi la Amkeni! linaelezwa kwenye ukurasa wa 4 wa gazeti hili: “La maana kuliko yote, gazeti hili hujenga uhakika katika ahadi ya Muumba ya kuleta ulimwengu mpya wenye amani na usalama.”

Broshua, Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje? imechapishwa ili kutimiza kusudi hilo. Unaweza kuomba nakala yako kwa kujaza kuponi iliyo hapa chini na kuituma kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni broshua Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje?

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki