Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 11/22 uku. 32
  • Kifo Chake Kiliombolezwa na Wengi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kifo Chake Kiliombolezwa na Wengi
  • Amkeni!—2002
Amkeni!—2002
g02 11/22 uku. 32

Kifo Chake Kiliombolezwa na Wengi

Mnamo Januari 12 mwaka huu, Jesse Barnes, aliyekuwa msimamizi wa idara ya umeme, alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata alipokuwa akifanya kazi katika jengo la serikali huko Washington, D.C. Alifanya kazi katika jengo hilo tangu mwaka wa 1995. Msimamizi mmoja alisema: “Kila mtu alimpenda Jesse.” Msaidizi wa msimamizi alisema hivi kumhusu Jesse: “Alikuwa mtu ambaye hata kama ulikutana naye mara moja tu, hungemsahau.” Kisha akaongeza: “Yeye hakuwalazimisha watu waamini mambo aliyoamini, lakini aliposikia watu wakitukana wengine, hakusita kuwaambia warekebishe mwenendo wao.”

Jesse, aliyekuwa Shahidi wa Yehova tangu mwaka wa 1993, alikufa akiwa na umri wa miaka 48. Maafisa wawili walimwalika mjane wake, Maureen, awatembelee, na alikutana nao katika Machi 20. Aliachia kila mmoja wao broshua iitwayo Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa na video Jehovah’s Witnesses—The Organization Behind the Name. Wanaume hao wawili walimshukuru kwa zawadi hizo. Mmoja wao alisema alithamini ziara yake sana kwa sababu baba yake alikuwa amekufa majuzi na haikuwa rahisi kukabiliana na hali hiyo.

Huenda wewe au mtu fulani unayemjua akafarijiwa na broshua hiyo yenye kurasa 32 Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa. Unaweza kuomba broshua hiyo kwa kujaza kuponi iliyo hapa chini na kuituma kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni broshua Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa.

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki