Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/11 uku. 32
  • Hekima ya Mfalme Sulemani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hekima ya Mfalme Sulemani
  • Amkeni!—2011
Amkeni!—2011
g 7/11 uku. 32

Hekima ya Mfalme Sulemani

● Mwalimu mmoja aliuliza wanafunzi wa darasa la nne wamweleze mambo waliyojua kumhusu Mfalme Sulemani anayetajwa katika Biblia. Sheena, msichana mwenye umri wa miaka tisa alisema kwamba alikuwa mfalme mwenye hekima sana na akaeleza jinsi alivyosuluhisha bishano kati ya wanawake wawili waliodai kuwa mama ya mtoto mmoja. Mwanzoni wanafunzi wenzake walishtuka sana waliposikia jinsi Sulemani alivyoshughulikia tatizo hilo, lakini mwalimu wake alisema kwamba alishughulikia jambo hilo kwa njia inayofaa.

Sheena alieleza kwamba alikuwa amejifunza hayo kutoka katika Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, kilicho na hadithi hiyo kuhusu hekima ya Sulemani. “Sita kati ya wanafunzi wenzangu waliomba nakala ya kitabu hicho cha Hadithi za Biblia,” akaeleza Sheena, kisha akasema: “Mwalimu wangu pia aliomba nakala moja. Hivyo kwa ujumla nilitoa nakala saba za kitabu hicho.”

Unaweza kuagiza nakala ya Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, kilicho na hadithi 116 zinazozungumzia watu na matukio ya Biblia. Unaweza kuomba kitabu hicho kwa kujaza sehemu iliyoonyeshwa hapa chini na kuituma kwa kutumia anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Bila masharti, ningependa kupokea kitabu kilichoonyeshwa hapa.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki