Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/13 kur. 12-13
  • Kutembelea Indonesia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Indonesia
  • Amkeni!—2013
Amkeni!—2013
g 4/13 kur. 12-13
[Picha katika ukurasa wa 12]

NCHI NA WATU

Kutembelea Indonesia

INDONESIA imefanyizwa na visiwa vipatavyo 17,000. Waindonesia wanajulikana kuwa watu wenye urafiki sana, wenye subira, adabu, na ukarimu.

[Ramani katika ukurasa wa 12]

Chakula nchini Indonesia kinatia ndani wali, vyakula vingine, na matunda. Mara nyingi wali na vyakula vingine hutiwa vikolezo. Katika maeneo fulani, familia huketi kwenye mkeka, na kula kwa kutumia vidole kuchovya vyakula vingine kwenye wali. Waindonesia wengi hudai kwamba chakula huwa kitamu sana kinapoliwa kwa njia hiyo.

[Picha katika ukurasa wa 13]

Tunda la duriani lina nyama yenye rangi ya malai na linapendwa na wengi licha ya harufu yake mbaya

Waindonesia wanapenda sanaa, dansi, na muziki. Anklong ni aina fulani ya ala ya muziki ya Indonesia; inatengenezwa kwa vipande vya mirija ya mianzi iliyoning’inizwa kwenye kiunzi. Mirija hiyo hupangwa katika njia ambayo itatokeza sauti mbalimbali inapotikiswa. Ili kucheza muziki, ni lazima wapiga ala washirikiane, kila mmoja akitikisa anklong yake kwa wakati barabara.

[Picha katika ukurasa wa 13]

Orangutangu—wanaopatikana katika misitu ya mvua ya Sumatra na Borneo—ndio wanyama wakubwa zaidi wanaoishi kwenye miti. Dume aliyekomaa anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 90.7 na mikono yenye urefu wa mita 2.4 kutoka upande mmoja hadi ule mwingine

Mpaka karne ya 15 W.K., Indonesia iliathiriwa sana na Uhindu na Ubudha. Kufikia karne ya 16, Uislamu ukawa umeathiri utamaduni wa Indonesia. Wazungu walipoenda huko katika karne ya 16 kutafuta vikolezo, waliingiza dini zilizodai kuwa za Kikristo nchini humo.

Mashahidi wa Yehova wanaojulikana ulimwenguni pote kwa sababu ya kazi yao ya kufundisha watu Biblia, wamekuwa wakifanya kazi hiyo nchini Indonesia tangu mwaka wa 1931. Kwa sasa, kuna Mashahidi wa Yehova zaidi ya 22,000 nchini Indonesia na wanajitahidi sana kuwafikia viziwi nchini humo. Hivi karibuni, zaidi ya viziwi 500 walihudhuria mkutano wa pekee wa lugha ya ishara uliofanywa na Mashahidi wa Yehova ili kuadhimisha kifo cha Yesu Kristo.

TAHINI UJUZI WAKO

Unafikiri Indonesia ina kitu gani kati ya vitu vifuatavyo?

  1. spishi 20,000 za mimea 

  2. idadi kubwa zaidi ulimwenguni ya wanyama wanaonyonyesha

  3. ua kubwa zaidi ulimwenguni

  4. ua refu zaidi ulimwenguni

JIBU: Yote manne. Ua kubwa zaidi ulimwenguni lina kipenyo cha sentimita 91, na ua refu zaidi lina kimo cha mita 3.

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya watu: 237,600,000

  • Mji mkuu: Jakarta

  • Hali ya hewa: Joto

  • Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi: Mafuta ya mawese, mpira, petroli, makaa ya mawe

  • Lugha zinazozungumzwa: Kibahasa cha Indonesia, pamoja na mamia ya lugha na lahaja zinazozungumzwa katika maeneo mbalimbali

  • Dini: Sehemu kubwa ni Waislamu (asilimia 88)

[Picha katika ukurasa wa 12]

Amkeni! huchapishwa katika lugha 98, kutia ndani Kiindonesia (lugha hiyo pia inaitwa Kibahasa cha Indonesia)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki