Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/14 kur. 12-13
  • Kutembelea Kambodia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Kambodia
  • Amkeni!—2014
Amkeni!—2014
g 4/14 kur. 12-13
Mashamba ya mpunga huko Kambodia

NCHI NA WATU | KAMBODIA

Kutembelea Kambodia

Ramani ya Kambodia

VIJIJI VINAVYOELEA, masoko yenye bidhaa nyingi, mitaa iliyojaa pikipiki zinazobeba kila kitu kuanzia kuku hadi friji—haya ni baadhi tu ya mambo unayoona na kusikia unapokuwa Kambodia.

Wakambodia wanajulikana sana kwa kuwa wachangamfu, wenye urafiki, na ushirikiano. Kwa kawaida wao huitana kaka, dada, shangazi, mjomba, bibi (nyanya), au babu—hata wanapokutana na mtu kwa mara ya kwanza!

Nyumba zilizojengwa juu ya maji

Baadhi ya Wakambodia huishi kwenye nyumba zinazoelea, na wengine kwenye nyumba zilizojengwa juu ya nguzo ndefu au juu ya mbao zinazoelea. Kuna shule, kliniki, masoko, na hata vituo vya mafuta vinavyoelea

Tunda linaloitwa Dragon

Matunda yanayoitwa Dragon yanapatikana huko Kambodia

Wali ni chakula kikuu cha Wakambodia. Mlo wa kawaida unakuwa angalau na aina tatu au nne za vyakula, mara nyingi supu haikosekani. Watu wengi wanapenda sana samaki. Kwa kawaida kila mlo huwa na mchanganyiko wa chakula kitamu, chenye uchachu, na chenye chumvi.

Miaka 2000 hivi iliyopita, wafanyabiashara kutoka India na watu waliokuwa wakisafiri kwenda China walipita kwenye pwani ya Kambodia na wakabadilishana bidhaa kama vile hariri na vito ili wapate vikolezo, miti yenye manukato, pembe za ndovu, na dhahabu. Baada ya muda Wakambodia waliiga tabia za India na China, na hivyo Uhindu na Ubudha ukasitawi nchini Kambodia. Leo, asilimia 90 ya watu wa Kambodia ni Wabudha.

Mashahidi wa Yehova wanahubiri ujumbe wa tumaini ulio katika Biblia nchini Kambodia. Wamewasaidia watu wengi kwa kutumia kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? Kitabu hicho kinapatikana katika lugha 250 hivi, kutia ndani Kikambodia.

Mashahidi wa Yehova wakimhubiria mwanamume Mkambodia ujumbe wa Biblia

Zaidi ya watu 1,500 nchini Kambodia wanajifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova na wanapata majibu ya maswali kama vile, “Wafu wako wapi?” na “Mungu ana kusudi gani kwa dunia?”

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya watu: Karibu milioni 14

  • Mji mkuu: Phnom Penh

  • Hali ya hewa: Joto la wastani na joto kali, pia msimu wa mvua na kiangazi

  • Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi: Nguo, mbao, mpira, mchele

Kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? cha Kikambodia

Kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa?, kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova, kinapatikana katika Kikambodia (kimeonyeshwa hapa).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki