Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/15 kur. 10-11
  • Kutembelea Uzbekistan

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Uzbekistan
  • Amkeni!—2015
Amkeni!—2015
g 10/15 kur. 10-11
Kuta za Itchan Kala Katika Khiva, Uzbekistan

Kuta za Itchan Kala katika Khiva

NCHI NA WATU

Kutembelea Uzbekistan

Ramani ya Uzbekistan

TRANSOXIANA. Nchi Katikati ya Mito. Tartary. Turkistan. Majina mengi yametumiwa ili kutambulisha eneo ambalo leo linatia ndani Uzbekistan, “Nchi ya Wauzbeki.” Tangu mapema karne ya 15, majiji ya Uzbekistan yaliwafaa wafanyabiashara waliosafiri katika barabara iliyounganisha China na Bahari ya Mediterania. Pamba hutumiwa zaidi katika viwanda vya nguo nchini humo. Mazulia mazuri yaliyotengenezwa kwa kutumia pamba, sufu, au hariri huuzwa pia.

Historia inaonyesha kwamba watu mbalimbali wamechangia utamaduni wa Uzbekistan. Watawala maarufu na majeshi yao yenye nguvu walipita katika milima na majangwa ya nchi ya Uzbekistan. Watu hao wanatia ndani Aleksanda Mkuu, aliyekutana na mpenzi wake Roxane; Genghis Khan, kutoka Mongolia; na Timur (anayejulikana pia kama Tamerlane), mwenyeji wa eneo hilo, aliyetawala mojawapo ya milki kubwa zaidi katika historia.

Wanaume wawili wamevaa nguo za asili za Wauzbeki

Nguo za asili

Minara yenye rangi zinazovutia yenye makuba yaliyofunikwa na vigae vyenye rangi ya bluu hufanya miji ya kisasa ya Uzbekistan ivutie. Majengo hayo mengi hutumiwa kama shule.

Barabara iliyounganisha China na Bahari ya Mediterania. Barabara hiyo ambayo inapita katika eneo ambalo leo ni Uzbekistan, ilikuwa maarufu sana katika ulimwengu wa biashara. Ilianza kutumiwa muda mrefu hadi njia mpya ya kwenda India kupitia bahari ilipofunguliwa mwishoni mwa karne ya 15 W.K.

Wanawake wawili wa Kiuzbeki wakitengeneza mazulia ya hariri

Kutengeneza mazulia ya hariri

Bahari ya Aral. Kwa kuwa mkondo wa maji ya Bahari ya Aral uligeuzwa na kutumiwa katika kilimo cha umwagiliaji—ambayo iliwahi kuwa ziwa la nne kwa ukubwa duniani—inaanza kutoweka. Nchi ya Uzbekistan inashirikiana na nchi zingine kutatua tatizo hilo.

Alfabeti za Uzbekistan zinazobadilika. Lugha mbalimbali zilitumiwa katika nchi hii lakini baada ya uvamizi wa Waislamu katika karne ya nane, Kiarabu kilianza kutumiwa. Baada ya nchi hii kuunga mkono Muungano wa Sovieti, alfabeti za Kilatini zilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na kisha herufi za Kisirili zikaanza kutumiwa mwishoni mwa miaka ya 1930. Mwaka wa 1993, sheria mpya iliyotungwa ilianzisha alfabeti za Uzbekistan inayotegemea maandishi ya Kilatini.

Matunda yaliyokaushwa katika soko nchini Uzbekistan

Kibanda cha matunda yaliyokaushwa katika soko

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya Watu: Milioni 30

  • Mji Mkuu: Tashkent

  • Hali ya Hewa: Kavu na mvua kidogo na unyevu kwa kiasi fulani

  • Nchi: Eneo tambarare kuelekea upande wa magharibi na milima kuelekea upande wa mashariki

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki