Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g17 Na. 5 kur. 14-15
  • Kutembelea Kazakhstan

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Kazakhstan
  • Amkeni!—2017
Amkeni!—2017
g17 Na. 5 kur. 14-15
Astana, Kazakhstan

Jiji la Astana

NCHI NA WATU

Kutembelea Kazakhstan

Ramani ya Kazakhstan

WAKAZAKH wa kale waliishi maisha ya kuhamahama. Hadi leo, baadhi ya Wakazakh ambao ni wafugaji huhama na makundi yao ya mifugo kulingana na majira. Wakati wa majira ya joto, wao hulisha mifugo katika maeneo yenye baridi ya nyanda za juu. Kisha, majira ya baridi yanapokaribia, wanapeleka mifugo yao katika maeneo ya chini yenye joto.

Baadhi ya Wakazakh wanaishi katika majiji ya kisasa. Hata hivyo, bado njia ya maisha ya mababu zao huonekana wazi katika utamaduni wao, vyakula, na sanaa. Wakazakh wana utajiri mwingi wa mashairi, nyimbo, na muziki ambao huchezwa kwa vifaa vya asili.

Yurt ni nyumba ya asili ya jamii zinazohamahama, ambayo inaweza kuhamishwa, nayo imekuwa ishara ya mtu anayeishi maisha ya asili. Wachungaji wanapenda kuishi kwenye yurt, nao Wakazakh wanaoishi mjini huitumia katika matukio ya pekee. Yurt hutumiwa pia kama makazi ya watalii. Sehemu ya ndani ya yurt huonyesha ustadi wa wanawake wa Kazakhstan katika kushona, kudarizi, na kufuma mazulia.

Familia ikiwa ndani ya yurt

Sehemu ya ndani ya yurt

Familia za Wakazakh wanaoishi mashambani huwathamini sana farasi wao. Kuna karibu majina 21 ya farasi katika lugha ya Kikazakh, kila moja likiwa na maana tofauti, na vilevile zaidi ya maneno 30 yanayofafanua aina za rangi ya manyoya ya farasi. Farasi ni zawadi ya bei ghali na inayothaminiwa sana. Katika maeneo ya mashambani, wavulana hujifunza kupanda farasi wakiwa na umri mdogo.

Kwa kawaida, chakula cha asili cha Wakazakh hutia ndani nyama isiyo na vikolezo. Wakazakh wanapenda sana koumiss, kinywaji ambacho hutengenezwa kutokana na maziwa ya farasi, na inasemekana kina faida nyingi za kiafya, na shubat, maziwa ya mgando yenye lishe yanayotokana na ngamia.

Watu wote wanakaribishwa kutembelea ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova iliyo katika mji wa Almaty.

Chui anayeishi kwenye theluji

Chui anayeishi kwenye theluji ambaye haonekani kwa ukawaida, huhamia juu kwenye milima ya Kazakhstan wakati wa majira ya joto

JE, WAJUA?

Kuna angalau aina 36 za maua mwitu ya tulipu nchini Kazakhstan, na mchoro wa maua hayo unatumiwa kwa ukawaida katika sanaa za asili za Wakazakh.

Ziwa Balkhash lililo nchini Kazakhstan lina maji yenye chumvi nyingi upande wa mashariki na yaliyo na chumvi kidogo sana upande wa magharibi.

Kuwinda kwa kutumia tai na ndege wengine bado ni utamaduni wa kawaida nchini Kazakhstan. Wakazakh wanawapenda sana tai wa dhahabu na wana ustadi mkubwa wa kuwazoeza kuwinda.

Tai aliyevishwa kiziba macho akiwa amesimama mkononi mwa mtu

Kifaa cha kufunika macho ya tai huwasaidia wasiwaogope wanadamu

  • LUGHA RASMI: KIKAZAKH, KIRUSI

  • IDADI YA WATU: 17,563,000

  • MJI MKUU: ASTANA

  • HALI YA HEWA: JOTO NA UKAME WAKATI WA KIANGAZI, THELUJI WAKATI WA MAJIRA YA BARIDI

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki