Wimbo 94
Mfalme wa Umilele, Litakase Jina Lako!
1. E Yehova, ni wewe tu,
Milele hubadiliki.
Wapenda na kusubiri,
Hata utakase jina.
Kusudilo la milele;
Unayo hekima nyingi;
Ufalme wako karibu,
Uovu wote uishe.
2. Muumba wa ulimwengu,
Ndiwe wa kale na kale!
Na umewaona watu,
Wazidi kuwa wabaya.
Ulitupa Mwana wako;
Ufalme wake wadumu.
Na adui wakimbia;
Twasali waharibiwe.
3. Na manabii wa kale
Walihubiri wokovu.
Unabii watimia,
Nasi tunashuhudia.
Dunia ni ya kudumu,
Milele Isitikiswe.
E Mufalme utukuke,
Uje Ufalme wa Kristo.