Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jv uku. 5
  • Dibaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Dibaji
  • Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
jv uku. 5

Dibaji

Mashahidi wa Yehova ni watu wanaojulikana sana lakini watu wengi hawawaelewi sana. Mahubiri yao na njia yao ya ibada imefikia vikundi vingi vya kitaifa na kikabila ulimwenguni pote, kutia ndani vijana na wazee, katika kila kiwango cha maisha na elimu. Bidii yao wakiwa wapiga-mbiu wa Ufalme wa Mungu imewavutia hata wachambuzi wao. Upendo wao kwa mmoja na mwenzake hufanya hata watu wasio Mashahidi watamani kwamba afadhali watu wengi zaidi wangependana hivyo.

Hata hivyo bado wengi hujiuliza, ‘Kwa kweli Mashahidi wa Yehova ni akina nani?’ Wengine wameandika juu yao, nyakati nyingine kwa kupendelea upande mmoja. Kwa kweli, wao wenyewe ndio wanaojua vizuri zaidi historia yao ya kisasa kuliko mtu mwingine yeyote. Wahariri wa buku hili wamejitahidi kutoa habari kwa jinsi ilivyo hasa na kutoa historia nyoofu. Kwa wote wanaojua yale ambayo Biblia hutabiri juu ya siku za mwisho, historia hii juu ya watu wanaoamini na kuhubiri sana yale ambayo Biblia husema, itakuwa yenye kusisimua kwelikweli.

Watangazaji

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki