Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • cl uku. 3
  • Utangulizi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Utangulizi
  • Mkaribie Yehova
Mkaribie Yehova
cl uku. 3

Utangulizi

Msomaji Mpendwa:

Je, unahisi ukiwa karibu na Mungu? Watu wengi wanadhani kwamba hilo haliwezekani kamwe. Baadhi yao hudhani kwamba Mungu hana hisia; wengine hujiona kuwa hawafai kabisa na hawawezi kamwe kumkaribia. Lakini, Biblia inatuhimiza hivi kwa upendo: “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia.” (Yakobo 4:8) Yeye hata anawahakikishia hivi wale wanaomwabudu: “Mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.”—Isaya 41:13.

Tunaweza kujitahidi jinsi gani kuwa na uhusiano wa karibu sana na Mungu? Ili kuwa na urafiki na mtu yeyote, ni lazima tumjue mtu huyo, tuvutiwe na sifa zake za pekee na kuzithamini. Hivyo basi, ni muhimu sana kwetu kujifunza kuhusu sifa na njia za Mungu za kutenda mambo, kama zinavyofunuliwa na Biblia. Tukitafakari juu ya jinsi Yehova anavyodhihirisha kila mojawapo ya sifa zake, jinsi Yesu Kristo alivyodhihirisha sifa hizo kikamili, na kufahamu jinsi sisi pia tunavyoweza kusitawisha sifa hizo, tutamkaribia Mungu zaidi. Tutaona kwamba Yehova ndiye Mwenye Enzi Kuu aliye halali na anayefaa wa ulimwengu wote mzima. Isitoshe, yeye ndiye Baba ambaye sote tunamhitaji. Akiwa mwenye nguvu, haki, hekima, na mwenye upendo, yeye hawaachi kamwe watoto wake waaminifu.

Kitabu hiki na kikusaidie kumkaribia Yehova Mungu zaidi, na kusitawisha uhusiano wa kudumu pamoja naye, ili uweze kuishi na kumsifu milele.

Wachapishaji

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki