Wimbo Na. 9
Msifuni Yehova Mungu Wetu!
Makala Iliyochapishwa
1. Sifuni Yehova Mungu!
Tangazeni jina lake!
Tangaza mwisho karibu,
Wote wasikie ujumbe.
Yehova Mungu ameagiza
Kwamba sasa ni wakati
Mwanaye atawale,
Tangaza baraka zake zijazo!
(Korasi)
Sifuni Yehova Mungu!
Tangazeni fahari yake!
2. Sifuni na kumwimbia!
Lisifuni jina lake!
Kwa shangwe, toka moyoni,
Utukufu wake tangaza.
Mungu ni mwema kwa watu wote,
Licha ya fahari yake.
Ni mwenye rehema na upendo.
Husikia tumwitapo.
(KORASI)
Sifuni Yehova Mungu!
Tangazeni fahari yake!
(Ona pia Zab. 89:27; 105:1; Yer. 33:11.)