Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 59 uku. 142-uku. 143 fu. 5
  • Wavulana Wanne Waliomtii Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wavulana Wanne Waliomtii Yehova
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Wavulana Wanne Babeli
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Watahiniwa—Lakini Wadumisha Uaminifu Kwa Yehova!
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Jinsi Kitabu Cha Danieli Kinavyokuhusu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Yehova Huthawabisha Imani na Ushujaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 59 uku. 142-uku. 143 fu. 5
Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria wanakataa kula chakula cha mfalme

SOMO LA 59

Wavulana Wanne Waliomtii Yehova

Nebukadneza alipochukua wana wa Yuda wa uzao wa kifalme hadi Babiloni, alimweka Ashpenazi, ofisa mkuu wa makao ya kifalme awatunze. Nebukadneza alimwambia Ashpenazi awatafute vijana wenye afya na sura nzuri zaidi kati yao. Vijana hao wangezoezwa kwa miaka mitatu. Mazoezi hayo yangewatayarisha kuwa maofisa wakuu nchini Babiloni. Wavulana hao walipaswa kujifunza kusoma, kuandika, na kuzungumza lugha ya Kiakadi iliyozungumzwa Babiloni. Walitarajiwa pia kula chakula kilekile ambacho mfalme na maofisa wake walikula. Wavulana wanne kati yao walikuwa Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria. Ashpenazi aliwapa majina ya Kibabiloni, yaani, Belteshaza, Shadraki, Meshaki, na Abednego. Je, elimu hiyo ingewafanya waache kumtumikia Yehova?

Wavulana hao wanne walikuwa wameazimia kumtii Yehova. Walijua kwamba hawakupaswa kula vyakula vya mfalme kwa kuwa Sheria ya Yehova ilisema kuwa baadhi ya vyakula hivyo vilikuwa najisi. Kwa hiyo, wakamwambia Ashpenazi hivi: ‘Tafadhali usitufanye tule chakula cha mfalme.’ Ashpenazi akawaambia hivi: ‘Mkikataa kula na mfalme aone kuwa mnaonekana wagonjwa, ataniua!’

Danieli alikuwa na wazo fulani. Akamwambia hivi mlinzi wao: ‘Tafadhali tupatie mboga za majani na maji tu kwa siku kumi. Kisha utulinganishe na wavulana wanaokula chakula cha mfalme.’ Mlinzi huyo akakubali.

Baada ya majaribio hayo ya siku kumi, Danieli na rafiki zake watatu walionekana wenye afya kuliko wavulana wengine wote. Yehova alifurahi kwamba walimtii. Hata akampa Danieli hekima ya kuelewa maono na ndoto.

Mazoezi hayo yalipoisha, Ashpenazi aliwaleta wavulana hao kwa Nebukadneza. Mfalme akazungumza nao na akaona kuwa Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria walikuwa na hekima na uelewaji zaidi kuliko wavulana wengine wote. Akawachagua wavulana hao wanne wafanye kazi kwenye makao yake ya kifalme. Mara nyingi, mfalme angewaomba ushauri kuhusiana na mambo muhimu. Yehova alikuwa amewapa hekima zaidi kuliko watu wote wenye hekima wa mfalme na wenye kufanya uchawi.

Ingawa walikuwa kwenye nchi ya kigeni, Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria hawakusahau kwamba walikuwa watu wa Yehova. Je, wewe pia utamkumbuka Yehova sikuzote, hata wakati ambapo wazazi wako hawatakuwa karibu?

“Usiruhusu kamwe mtu yeyote audharau ujana wako. Badala yake, uwe mfano mzuri kwa waaminifu katika kusema, katika mwenendo, katika upendo, katika imani, na katika usafi wa kiadili.”​—1 Timotheo 4:12

Maswali: Kwa nini Danieli na rafiki zake watatu walimtii Yehova? Yehova aliwasaidia jinsi gani?

Danieli 1:1-21

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki