ANIMU
(Animu).
Jiji lililokuwa katika eneo lenye milima kusini mwa Yuda linalotajwa wakati wa mgawanyo wa maeneo katika siku za Yoshua. (Yos 15:48, 50) Linahusianishwa na Khirbet Ghuwein et-Tahta (Horvat ʽAnim), magofu yanayopatikana km 5 hivi Ks mwa Eshtemoa na km 19 hivi Ks-Ks-Mg mwa Hebroni